Ticker

7/recent/ticker-posts

MWANAUME KUSUKA NYWELE ZANZIBAR NI TSH. MILIONI MOJA

Kiasi cha Shilingi milioni moja kitatozwa kwa mwanaume atakayetaka kusuka nywele zake.

Uamuzi huo umelenga  kuutokomeza mtindo wa wanaume kusuka nywele, visiwani humo.

Kwa mujibu wa Katibu- Mtendaji wa Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar, Dkt.Omar Adam si utamaduni wa mzanzibari kwa mwanaume kusuka nywele.

Alisema mwanaume yeyote aliyesuka nywele na hana kibali maalum cha kufanya hivyo, atakamatwa.

"Askari wanakamata wanaume wote wanaosuka nywele kama za wasichana, Baraza la Sanaa hatupendelei kuona hilo kwa sababu si utamaduni wetu.

" Kuna kibali maalum cha kusuka nywele kwa wanaume ambacho shilingi milioni moja.

"Tumeweka bei hiyo ili kuwakomoa, sasa utachagua mwenyewe utoe milioni moja usuke au ununue kiwembe chako cha Shilingi 100 unyoe," alisema Dkt. Omar.

Post a Comment

0 Comments