Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mary Masanja amewatahadharisha Wananchi Mkoani Iringa kuwa na tahadhari na kuacha kutembea usiku ili kuepuka kuvamiwa na Simba walioingia katika makazi ya watu.
“Niendelee kutoa elimu kupitia Bunge hili kwamba wakati huu ambapo tunawasaka hawa Simba wananchi wawe na tahadhari ya kutotembea usiku, lakini pia wenye mifugo wawashe moto kuzunguka maeneo ya mifugo yao ili kuepusha Simba wasiwasogelee.”
Kufuatia hatua hiyo.
Masanja amesema Serikali tayari imeshapeleka helikopta inayozunguka usiku na mchana kuhakikisha Simba hao wanapatikana na kurudishwa katika maeneo yao ili kuhakikisha maisha ya Watanzania yanalindwa kwa gharama yoyote
0 Comments