Ticker

7/recent/ticker-posts

CHALAMILA AWATOLEA UVIVU WATENDAJI NA MADIWANI KIGAMBONI

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewataka watendaji wa wilaya ya  Kigamboni kufanya kazi ili  akiwakanyaga wasikimbilie kusema ana vyeti feti.

Akizungumza katika ziara ya Kikazi wilayani humo, Chalamila amesema Rais Samia Suluhu Hassan anategemea watendaji wafanye kazi na ili kutimiza hilo ni muhimu kujua Rais anataka nini.

"Nikawakanyaga kanyaga hamkawii kusema Mkuu wa Mkoa ana vyeti feki, hapana vyangu ni halisia (original)," Chalamila amesema. "Kikubwa ambacho tunahitaji ni ushirikiano, wanasema mtu mmoja hawezi kuongoza ila kwa pamoja tunaweza kuongoza."

Chalamila amesisitiza kuwa ni lazima kuboresha mahusiano ili kushirikiana kwa pamoja.

"Nimesikia ninyi madiwani baadhi yenu ni tatizo kuna wakati miradi inakwama eti kwa kugombea mgao wa asilimia 10, sasa nitakuwa natumia vyombo kuwachunguza na ikibainika tutawakamata baadhi ili iwe fundisho," ameonya Chalamila

Post a Comment

0 Comments