Ticker

7/recent/ticker-posts

BAKWATA YAISHAURI SERIKALI KUTOA ELIMU KWA WANANCHI JUU YA MKATABA WA BANDARI

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA limeishauri serikali kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mkataba wa Serikali ya Tanzania na kampuni ya DP World wa uendeshaji wa Bandari.

Bakwata imeishauri Serikali kuwaeleza Watanzania  faida zitakazopatikana kupitia uwekezaji huo, pamoja na kusikiliza maoni ya wananchi, ikiwa pamoja na kufanyiakazi vipengele vyenye ukakasi katika mkataba huo

Hayo yamesemwa leo Juni 29,2023 na Katibu Mkuu wa BAKWATA Alhaj Sheikh Nuhu Mruma katika baraza la Eid el-adh'haa lililofanyika  katika msikiti wa Mfalme Mohamed VI Kinondoni, Dar es Salaam 

"Kipekee tunampongeza sana Rais Samia kwa kuendesha serikali yake kwa uwazi kiasi mkataba huu kuweza kujadiliwa na wananchi," amesema. 




Post a Comment

0 Comments