Ticker

7/recent/ticker-posts

RAIS DKT.MWINYI AONESHWA NOTI YA ZANZIBAR ILIYOTUMIKA MWAKA 1916

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa  na mke wake Mama Mariam Mwinyi na ujumbe wake, walipata fursa ya kutembezwa ndani ya makumbusho makubwa mjini Doha yemye mkusanyiko mkubwa wa vitu vya kihistoria kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

Moja kati ya vitu vilivyomvutia Rais Mwinyi kwenye makumbusho hayo ni noti ya zamani ya Zanzibar iliyotumika mwanzoni mwa mwaka 1916. 

Kukuta noti hiyo katika makumbusho ya nchi ya Qatar kunadhihirisha ushawishi na utajiri wa historia ya Zanzibar na thamani yake katika historia ya dunia.


Mbali na noti hiyo, makumbusho hayo pia yanahifadhi aina mbalimbali za magari ya zamani, yakiwemo yale yaliyotengenezwa mnamo mwaka 1890

Kabla ya kutembelea makumbusho hayo Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi alihudhuria dhifa ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Mfanyabiashara maarufu kutoka Qatar Feisal Bin Qassim Bin Feisal Bin Thani Bin Qassim Bin Mohamed Al Thani. Mfanyabiashara huyu pia ndie mmiliki wa hoteli 30 kubwa duniani na makumbusho hayo aliyoyatembelea Rais Dkt. Mwinyi.







Post a Comment

0 Comments