Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko mengine ya wakuu wa mikoa pamoja na kuteua Mkuu wa mkoa na Mkuu wa wilaya mpya.
Mabadiliko haya ni ya pili ndani ya mwezi huu wa Mei, ambapo Mei 15,2023 alianza kwa kumhamisha Amos Gabriel Makalla kutoka Dar es Salaam na kumpeleka mkoa wa Mwanza.
Adam Kighoma Malima alihamishiwa mkoani Morogoro akitokea mkoa wa Mwanza.
Fatma Abubakar Mwassa alihamishiwa Mkoa wa Kagera akitokea mkoa wa Morogoro.
Albert John Chalamila alipelekwa mkoa wa Dar es Salaam akitokea mkoa wa Kagera.
Katika mabadiliko ya leo Mei 23,2023 Rais Samia amesema atampangia kazi nyengine aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Generali Sulemani Mungiya Mzee na nafasi yake kijazwa na Said Mohamed Mtanda ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo.
Nafasi ya Mtanda imejazwa na Kenani Kihangosi.
Aidha amemuhamisha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Queen Sendiga kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
Charles Makongoro Nyerere aliyekuwa akiuongoza mkoa wa Manyara amepelekwa mkoani Rukwa kuendelea na wadhifa wake wa Mkuu wa Mkoa.
Taarifa ya Mkurigenzi wa Mawasiliano y Rais, Ikulu, Zuhura Yunus imeweka wazi kuwa mabadiliko, uhamisho na uteuzi huo umeanza mara moja na uapisho wa Mkuu mpya wa Mkoa utafanyika kesho, Ikulu Chamwino, jijini Dodoma.
0 Comments