Ticker

7/recent/ticker-posts

NAPE AIONGEZEA MUDA KAMATI YA KUTATHIMINI UCHUMI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ameiongezea muda wa miezi sita Kamati Maalum  iliyopewa jukumu la kutathmini hali ya uchumi wa vyombo vya Habari na wanahanari nchini.

Waziri Nape aliunda Kamati hiyo Maalumu na kuitangaza Kwa wanahanari Januari 24,2023.

Akizungumza leo Mei 23,2023  na Waandishi wa  Habari jijini Dodoma, waziri Nape ameona haja ya kuiongezea  muda wa miezi sita.

Kamati hiyo inaongozwa na Mwenyekiti Tido Mhando na Katibu wake ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa.


Kamati hiyo inaundwa na watu tisa wengi wao wakiwa ni wanahabari kitaaluma.

Post a Comment

0 Comments