Mahakama ya wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, imemuhukumu Muharami Hassan Nayonga, kifungo cha miaka 30 jela baada ya kumkuta na hatia ya kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile na wanaume wenzake.
Muharami ambaye anatajwa kuwa ni mlinzi wa SUMA JKT na mkazi wa Kata ya Masoko, alikamatwa Aprili 13, 2023, baada ya kumshawishi kwa kutumia simu, kijana anayefahamika kwa jina la Zalafi Selemani ili akamuingilie kinyume na maumbile.
Baada ya kukamatwa, mtuhumiwa alichunguzwa na wataalamu wa Afya ambao walibaini kuwa kijana huyo hufanya ngono kinyume na maumbile.
0 Comments