Vinywaji vinavyodaiwa kuongeza nguvu mwilini (energy drink) ambavyo vimekuwa viburudisho vikubwa kwa vijana, Sasa rasmi ni hatari Kwa afya.
Katika siku za karibuni kumeibuka wimbi kubwa la vijana kupenda kutumia vinywaji hivyo Kwa hoja kuwa vinawaondolea uchovu na kuwafanya kuwa na nguvu zaidi.
Hata hivyo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imebaini kuwa vinywaji hivyo vina athari mbaya kwenye chembe chembe za damu hali inayofifisha utendaji kazi wa mwisho wa damu.
Hatua hiyo ya kufifisha utendaji wa kazi wa damu unasababisha kuganda kwa damu.
Kitendo cha kuganda kwa damu kunaibua hatari ya kuzuia mzunguko wa damu mwilini.
Tahadhari imetolewa kwa watumiaji kuacha ama kupunguza kwa kiasi kikubwa.
0 Comments