Ticker

7/recent/ticker-posts

‘WANAWAKE MSIWEKE TUMBAKI SEHEMU NYETI’

Tumbaku
DAKTARI Bingwa wa Magonjwa ya wanawake na Saratani kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando, Amina Yusuph amewaonya wanawake hasa wa kanda ya Ziwa kuacha tabia ya kuweka tumbaku kwenye sehemu zao za siri.

Imeelezwa kuwa wapo baadhi ya wanawake wanaweka tumbaku kwenye sehemu zao za siri ili ili kupata msisimko kimwili na kuamsha ari ya tendo la ndoa.

Dkt. Amina amesema kufanya hivyo kunawaweka kwenye hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi.

“Asilimia 80 ya wakina mama wanaokuja kupima saratani ya mlango wa kizazi hukutwa wamepakia tumbaku ukeni, kitendo hiki sio sahihi na ni hatari.” 

Post a Comment

0 Comments