Ticker

7/recent/ticker-posts

CHAMA, MAYELE, INONGA WAONDOKA

 

WACHEZAJI wa kimataifa wa timu za Simba na Yanga  Clatous Chama, Fiston Mayele, Kennedy Musonda na Henock Inonga wameondoka leo kwenda kutumikia nchi zao kwenye michuano ya kimataifa inayohusisha timu za Taifa.

Wachezaji hao wamekutana leo kwenye  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Chama na Musonda  wanaelekea Zambia, wakati Mayele na Inonga wao wanakwenda Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo  (DRC) Congo. 

Wachezaji hao wanaenda kuchezea nchi zao katika michuano ya kuwania kufuzu fainali za Afrika (AFCON).


Post a Comment

0 Comments