Ticker

7/recent/ticker-posts

LATRA YASHIRIKI MAPAMBANO DHIDI YA AJALI ZA BARABARANI

 LATRA YASHIRIKI MAPAMBANO DHIDI YA AJALI...

 

Moja ya ajali za barabarani
NA MWANDISHI WETU

 

KATIKA kuhakikisha ajali zinapungua n ahata kuisha kabisa nchini Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imeamua kutumia nguvu zake kikamilifu kwa kusitisha leseni za usafirishaji abiria kwa mabasi 22.

 

Mabasi hayo yamewekwa nje ya barabara kwa kipindi cha mwezi mmoja, ambapo adhabu hiyo ilishaanza kutekelezwa tangu Januari mwaka huu na itafikia tamati mwishoni mwa mwezi huu.





Mkurugenzi wa LATRA, Johansen Kahatano

 Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa LATRA, Johansen Kahatano amesema hatua hiyo ya kusitisha leseni hizo ilitokana na Mabasi hayo kuingilia Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Magari (VTS).

 

“LATRA tumechukua hatua ya kusitisha leseni kwa mabasi 22 baada ya kufuatilia na kubaini kuchezea mifumo kwa kuchezea vifaa vyake na kuviharibu kwa kubadilisha mifumo ya umeme.”

 

“Kuingilia Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Magari (VTS) ni kinyume na Kanuni ya 51 ya Kanuni za Leseni za Usafirishaji (Magari ya Abiria) za mwaka 2020. Hivyo, Mamlaka imechukua hatua hiyo ya kusitisha Leseni kwa mujibu wa Sheria ya LATRA ya mwaka 2019 na Kanuni zake za mwaka 2020.”

Kahatano ametoa ombi kwa wananchi wote kutoa taarifa kwa Mamlaka husika za usafiri ili kuchukuliwa hatua stahiki kwa madereva wanaoendesha wasiofuata utaratibu.

 

Aidha amesema hadi sasa LATRA imesajili madereva 13,291 na tayari Madereva 904 wamefanya mitihani ya kuthibitishwa na Mamlaka hiyo.

 

LATRA inatoa wito kwa Wamiliki wa Mabasi yanayotoa huduma za kibiashara kuhakikisha Madereva wao wanafika kwenye Ofisi za LATRA, Tanzania Bara ili kusajiliwa na mwisho wa usajili ni Aprili 30, 2023.

Post a Comment

0 Comments