Ticker

7/recent/ticker-posts

MFUMO WA NYUMBA JANJA KUPUNGUZA MATUMIZI YA UMEME


Na Mwandishi Wetu

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), limekuja na teknolojia ya Nyumba Janja ambayo itarahisisha usalama na kudhibiti wa vifaa vya umeme majumbani.

Hayo yamesemwa na Ofisa Masoko wa TANESCO, Madelaine Shaidi wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam.

Shaidi alisema teknolojia imekuwa kwa kasi, hivyo TANESCO imekuja na mfumo ambao unaweza kuunganisha vifaa vya umeme kupitia ufungaji wa soketi za kidigitali.

Alisema teknolojia hiyo inahitaji jubadilisha soketi pekee na sio mfumo wa umeme, hali ambayo itampunguzia gharama mwenye nyumba.

"Tumekuja na mfumo ambao mwemye nyumba anaweza kuwasha na kuzima vifaa vya umeme kwa muda anaotaka vitumike. Kubwa zaidi kupitia teknolojia hiyo inaonesha matumizi ya umeme kila siku na kifaa gani kinatumia umeme zaidi," alisema.

Ofisa huyo ametaja vifaa ambavyo vinaweza kuunganishwa na mfumo huo ni friji, pasi, TV, AC na vingine. Alisema mfumo huo unaenda kutoa malalamiko ya umeme kuisha bila taarifa sahihi na kuzuia ajali za moto kwani mmiliki anaweza kudhibiti.

Shaidi alisema mfumo huo unatoa fursa kwa mmiliki kupanga taa ziwake na kuzima saa ngapi. Ofisa huyo ametoa rai kwa wananchi kufunga mfumo huo ambao ni rafiki kiuchumi na kiusalama. Alisema TANESCO ina wataalam ambao wanaweza kufunga mfumo huo, hivyo wananchi wafike kwenye ofisi zao ili kupata huduma hiyo ya kisasa.

"Fungeni sekote za nyumba janja zina faida sana hasa kwenye matumizi na usalama wa nyumba.




Post a Comment

0 Comments