Ticker

7/recent/ticker-posts

BIFU LA ALI KIBA NA DIAMOND NI AFYA KWA BONGO FLEVA

Diamond...
Katika historia ya muziki wa Bongo fleva, kumekuwa na vipindi ambavyo ushindani kati ya wasanii wakubwa umechochea ubunifu, ubora na ukuaji wa muziki kwa kasi ya ajabu. 

Miongoni mwa mifano hai na inayoendelea kuandika historia hiyo ni mvutano (bifu) kati ya Alikiba na Diamond Platnumz, ushindani ambao, badala ya kuharibu tasnia, umeigeuza kuwa jukwaa la ubora na mafanikio makubwa ndani na nje ya Tanzania.

Kauli ya Kiba  kuwa bora dhidi ya wengi Baada ya show yake kali Rock City, Mwanza, Alikiba alitoa kauli nzito:"Watatoa ngoma nyingine na nyingine… halafu mimi natoa nyingine, moja tu."

 Kauli hii si ya kubeza bali ni msimamo wa kisanii unaoonesha falsafa yake, kuweka mkazo kwenye ubora wa kazi badala ya wingi. 

Ali Kiba


Hapa ndipo tofauti ya kimkakati kati yake na Diamond inapojitokeza wazi. Mitazamo miwili, mafanikio tofauti kwa zaidi ya miaka 20, Alikiba amejijenga kama msanii wa hisia, ‘strong vocalist’, mwandishi mzuri na performer anayethamini sana live band. 

Muziki wake una maisha marefu (timeless), unaogusa nafsi na kudumu kwa muda mrefu sokoni.

Kwa upande mwingine, Diamond amejiweka kama mburudishaji ‘entertainer’ kamili anayechanganya uimbaji, dansi na ubunifu wa kisasa. 

Ana uwezo mkubwa wa kutengeneza nyimbo “catchy” zinazoendana na wakati husika huku akiwa na nguvu kubwa kwenye majukwaa ya kidigitali na mitandao ya kijamii.

Kwa lugha rahisi Kiba ni mwanamuziki mwenye  ubora wa kudumu (quality & longevity) huku Diamond akiwa ni mwanamuziki mwenye uwezo wa kushika soko (trend & consistency) 

Ali Kiba
Tofauti hizi si udhaifu, bali ndizo nguvu zinazolifanya bifu lao liwe na maana zaidi na ndio maana haitakuja kutokea wawili hawa wakashikana mashati ama kurushiana matusi.

Ushindani unaoinua viwango ukweli usiopingika ni kwamba ushindani wao umeongeza kiwango cha muziki wa Tanzania. Kila mmoja analazimika kuboresha sauti na maandishi yake, kuongeza ubunifu wa video, kuwekeza kwenye performances na kufikiria soko la kimataifa. 

Matokeo yake ni Bongo Flava imevuka mipaka ya Afrika Mashariki na kuwa sehemu ya mazungumzo ya muziki Afrika na duniani.

Mfano mzuri ni wimbo wa “Finale” wa Alikiba akiwa na Bien, ambao umeonesha jinsi wasanii wa Tanzania wanavyoweza kushirikiana kimataifa huku wakibeba ushindani wao wa ndani kama motisha ya kufanya vizuri zaidi.

Bifu kama chombo cha ukuaji kitaalamu, ushindani (competitive rivalry) ni injini ya ubunifu. Bila presha ya kushindana wasanii hupoteza ari ya kujiboresha, soko hupungua ubunifu na mashabiki hupoteza hamasa. 

Hivyo basi, bifu la Kiba na Diamond limekuwa kama “benchmark” ama tuseme ni kipimo cha ubora kwa wasanii wengine wanaochipukia.

Diamond Platnamz
Kisa cha Marioo na changamoto ya kukosa mpinzani Marioo ni mfano hai wa msanii mwenye mafanikio makubwa ya karibuni, ameonyesha consistency ya hits na ubunifu mkubwa. Hata hivyo, mjadala wake unakuwa mgumu kwa sababu hana mpinzani wa moja kwa moja kama ilivyo kwa Kiba na Diamond.

Hii inaonesha jambo muhimu kuwa ushindani wa wazi huongeza hadhi ya msanii na kumjengea simulizi (narrative) inayomuweka juu zaidi sokoni.

Athari Chanya kwa Afrika kupitia ushindani huu muziki wa Tanzania umeongeza hadhi barani Afrika, wasanii wanashindana kimataifa (Nigeria, Afrika Kusini na kwingineko),ubora wa production umeongezeka na audience imepanuka kupitia digital platforms. 

Kwa kifupi, bifu lao limekuwa daraja la kuipeleka Bongo Flava kwenye ramani ya dunia, Bifu lao si ugomvi wa kawaida wa wasanii ni mfumo wa ushindani unaoleta mageuzi. Ni vita ya kimkakati kati ya ubora na wingi, kati ya legacy na trend.

Na mwisho wa yote, mshindi mkubwa si Kiba wala Diamond, mshindi ni muziki wa Bongo Flava wenyewe.

Marioo...

 
 
 
 
 
 
 
 

 

Post a Comment

0 Comments