Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan |
NA MWANDISHI WETU
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na taarifa za mauaji ya Mjumbe wa Sekretariet Taifa ya Chama cha Demokrasia na Maendelo (Chadema) ambae pia ni msaidizi wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Ali Kibao.
Taarifa za kifo cha Mzee Kibo zilisambaa mwishoni mwa wiki iliyopita huku ikielezwa kuwa mwanasiasa huyo alitekwa na baadae mwili wake kupatikana ukiwa na majeraha mengi.
Kutokana na kuguswa na kifo hicho, Rais Samia ametoa maagizo kwa vyombo vya uchunguzi kumpelekea taarifa ya kina juu ya tukio hilo.
“Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa CHADEMA, Bwana Mohamed Ali Kibao. Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki.
"Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii.” amesema Rais Samia.
0 Comments