Ticker

7/recent/ticker-posts

AJALI YA CHOPA YAUA MKUU WA JESHI LA KENYA

Hayati Generali Francis Ogolla.

ARINEWSSWAHILI-KENYA

Ni huzuni nchini Kenya baada ya alasiri ya leo Aprili 18,2024 kutokea kwa tukio la ajali ya Chopa iliyochukua uhai wa Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF), Generali Francis Ogolla.

Chopa hiyo ilianguka na kuwaka moto katika eneo la Kaber, Wadi ya Endo, Elgeyo Marakwet, muda mfupi baada ya kuondoka katika Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Cheptuel Alasiri ya leo.

 

Taarifa kutoka NTV zinaonyesha kuwa mamlaka imethibitisha kufariki dunia kwa watu watano katika ajali hiyo mbaya, huku watu watatu wakinusurika. 

 

Viongozi hao walikuwa wakifanya ziara ya kutathmini hali ya usalama na kujadili uwezekano wa kufunguliwa kwa shule katika eneo la mpaka kati ya Pokot Magharibi na Elgeyo Marakwet.

 

Sehemu ambayo Chopa hiyo ilipoangukia.

Post a Comment

0 Comments