Ticker

7/recent/ticker-posts

LATRA YAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WA HABARI

NA FATMA JALALA-AFRINEWSSWAHILI-PWANI
MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imewapa semina ya kuwajengea uelewa zaidi mabalozi ambao ni waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam.

 Semina hiyo ya siku mbili imeanza Februari 26,2024  katika hoteli ya Njuweni Kibaha Pwani, semina hiyo  imefunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya LATRA  Wakili Tumaini Slaa.

 

Aidha,Wakili Slaa amewaasa Mabalozi hao kuwa na umakini na Uzalendo katika uandishi  wa habari za Mamlaka hiyo, pia amewataarifu kuwa bodi iko bega kwa bega nao na inafuatilia habari zinazotolewa nao, na katika kithibitisha hayo bodi imetoa maelekezo kwa watendaji wa Mamlaka kutoa ushirikiano wa kutosha na  taarifa pindi wanapozihitaji.

 

Pia Wakili Slaa amewasihi mabalozi hao kuwa wazalendo wanapoandika taarifa za Mamlaka kwani kwa kuzingatia uzalendo huo hali ya nchi itakuwa salama,  "mkiandika habari mbaya na zenye mazingira mabaya kwa jamii mtahatarisha usalama wa nchi yetu, hivyo hakuna atakayebaki salama,

bali habari hizo zikiandikwa vizuri na kwa kuzingatia weledi na uzalendo basi kila mmoja atakuwa salama,kwani maneno amani na uzalendo unaweza kuona ni vitu vidogo tu kwa kuviongea ila ni vitu vikubwa sana na vya msingi nchini.

Post a Comment

0 Comments