Ticker

7/recent/ticker-posts

AJALI YA MOTO KENYA, RAIS RUTO AWATAKA MAWAZIRI WAKE KUWAJIBIKA

Rais wa Kenya, William Ruto ametaka kuwajibishwa kwa baadhi ya maofisa wa serikali pamoja na baadhi ya mawaziri kuwajibika kutokana na ajali ya moto iliyotokea hivi karibuni. 

Rais Ruto ambae ameoneshwa kukerwa na ajali hiyo, pia amewalaumu baadhi ya Maafisa wa Serikali na kueleza kuwa uzembe na Rushwa vimesababisha mlipuko wa Gesi uliotokana na Lori lenye mitungi kulipuka katika Mtaa wa Embakasi, Februari 1, 2024 Jijini Nairobi na kuua Watu watatu na kujeruhi wengine 280.

Rais ametamka wazi kuwa kuna haja ya kufukuzwa kazi kwa Maafisa waliohusika kuruhusu eneo hilo kutumika kuhifadhi Gesi kinyume cha Sheria na kuwa Mawaziri wanaohusika na sekta husika wachukue hatua kwa kuwa kuna mazingira ya kukosekana kwa uwajibikaji Taarifa za awali zilieleza kuwa mlipuko ulitokea katika ghala lililo karibu na makazi ya watu ambalo lilizuiwa kutumika Mei 2023 na kwamba kuna Maafisa wanne wa Serikali walitoa leseni bila kuheshimu taratibu.

Post a Comment

0 Comments