Ticker

7/recent/ticker-posts

TANTRADE YAWAUNGANISHA WAFANYABISHARA WA TANZANIA NA INDONESIA, YAAHIDI KUENDELEA KUIBUA FURSA ZAIDI

JARKARTA,INDONESIA

Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ilioanza Januari 24, 2024 yenye lengo la kuendeleza na kukuza mahusiano ya kiuchumi kati ya Tanzania na Indonesia yenye kuhamasisha biashara na Uwekezaji kwa pande zote mbili, imekuwa ya mafanikio makubwa.

Miongoni mwa mafanikio hayo ni hatua ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)  kuratibu na kushiriki kwenye  Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Indonesia lililofanyika Januari 25, 2024 katika jiji la  Jakarta.

Katika kongamano hilo, taasisi mbalimbali za  Sekta Binafsi na Umma pamoja na wafanyabiashara kutoka Tanzania wamekutana na wenzao wa Indonesia na kubadilishana fursa za kibiashara.


Katika kudhihirisha kuwa ana nia ya kufungua milango ya kibiashara, Rais Dkt.Samia amewahakikishia wafanyabiashara wa  Indonesia na Tanzania mazingira mazuri yatakayoendelea kukuza  biashara baina ya nchi hizi mbili ikiwa ni pamoja na sera thabiti za kisiasa na uchumi.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bi. Latifa Mohamed Khamis pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa PT PPI, Soegeng Hernowo walisaini na kubadilishana Hati ya makubaliano ya ushirikiano katika ukuzaji biashara kwa nchi zote mbili. 

Bi. Latiba alitumia fursa hiyo kuainisha fursa za biashara zilizopo Tanzania na kueleza kuwa TanTrade itaendelea  kuibua fursa kwa wadau wa biashara nchini na kuratibu mikutano ya Biashara na kuhakikisha wafanyabiashara wa Tanzania wanaunganishwa na wafanyabiashara wa Indonesia ili kupata soko la bidhaa zinazozalishwa niching.





Post a Comment

0 Comments