Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo Desemba 6, 2023 amewatembela na kuwajulia hali majeruhi wa maafa ya mafuriko ya matope na mawe yaliyotokea Wilaya ya Hanang mkoani Manyara ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.
Dkt. Tulia ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuharakisha zoezi la kuwahudumia majeruhi hao. Aidha ameipongeza timu ya madakatri waliotoka Mikoa ya jirani kufika mapema katika Hospitali hiyo na kuongeza nguvu ya kutoa huduma.
0 Comments