Ticker

7/recent/ticker-posts

MELI KUBWA YA KITALII YATIA NANGA ZANZIBAR IKIWA NA KUNDI LA WATALII

Kishindo cha filamu ya Royal Tour iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, kimeendelea kutikisa kwenye sekta ya utalii nchini, ambapo sasa idadi kubwa ya watalii wanaingia nchini.

Jana Desemba 16,2023 meli kubwa ya kitalii ya Silver Spirit iliyobeba jumla ya watalii 432 na wafanyakazi wa meli 402 ilitia nanga kwenye Bandari ya Zanzibar. 

Meli hiyo imetoka nchini Usheli sheli na baada ya kutoka Zanzibar itakwenda Madagascar.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Dkt. Abdulla Mohamed Juma, ujio wa meli hiyo ni mwendelezo wa ujio wa meli za kitalii Zanzibar.

Dkt. Abdulla Mohamed Juma amempongeza Rais Samia kwa kufanya filamu ya Royal Tour ambayo imeongeza Kasi ya ujio wa Watalii nchini.

Mkurugenzi huyo alisema Wizara ya Utalii Zanzibar Kwa kushirikiana na ile ya bara wamekuwa wakifanya kila namna sahihi Ili kuwavutia Watalii zaidi.


Post a Comment

0 Comments