Ticker

7/recent/ticker-posts

SHAMBA BOI AHUSISHWA NA MAUAJI YA MAMA NA MTOTO MOROGORO

Mwanamama Mwanaisha Matere (37) na mwanae Baraka Maita mwenye umri wa miaka 7 wote ni wakazi wa Kijiji cha Mavimba Kata ya Milola Wilayani Ulanga Mkoani Morogoro, wameuawa kwa kuchinjwa na kutenganishwa viwiliwili vyao na vichwa.

Hadi sasa chanzo cha mauji hayo  bado hakijafahamika na Diwani wa Kata ya Milola lilikotokea tukio hilo Masoud  Mohamedi amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Novemba 24,2023.

Majirani ndio waliona damu zikichuruzika mlangoni na walipofungua mlango walikuta viwiliwili vya marehemu vikiwa havina vichwa.

Amesema katika nyumba hiyo walikuwa wakiishi na Mtu mmoja Mgeni ambaye alikaribishwa kama Mfanyakazi wa shamba lakini baada ya tukio hilo hakuonekana nyumbani hapo na wakati tukio linatokea Baba wa familia hiyo alikuwa amesafiri na kuwaacha nyumbani hapo Mke, Mtoto wake pamoja na Mgeni huyo ambaye anahisiwa kuwa ndiye aliyewaua na kuwakata vichwa mama na mtoto kisha kuondoka na vichwa.

Mkuu wa Wilaya ya Ulanga , Julius Ningu amethibisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema jitihada zinaendelea za kumsaka mtuhumiwa.

Post a Comment

0 Comments