Ticker

7/recent/ticker-posts

MUSWADA WA BIMA YA AFYA KURUDI BUNGENI KESHO

Wizara ya Afya kesho Novemba1,2023  inatarajia kurejesha Bungeni Muswada wa Bima ya Afya kwa wote ambao ulikwama Mwezi Februari 2023 kwa hoja iliyotolewa na Bunge ya kutokuwepo kwa chanzo endelevu cha fedha za kutekeleza mpango huo.

Muswada huu ni ndoto ya Serikali ya miaka mingi ambapo Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeboresha huduma bora za afya kuanzia ngazi ya Taifa hadi ya msingi kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya karibu zaidi na maeneo yao.

“Serikali kupitia Wizara ya Afya, Wadau wa Sekta na Wataalam wengine tayari wamefanyia kazi hoja zote zilizoibuliwa na Bunge pamoja na Wadau, hata hivyo semina zimefanyika kwa makundi mbalimbali ndani ya jamii kuhusu umuhimu wa Bima ya Afya kwa wote na tulipokea maoni yao na kuyafanyia kazi wananchi kesho watege macho na masikio yao Bungeni kujua nini ambacho Waziri wa Afya Mheshiwa Ummy Mwalimu atawasilisha Bungeni” Amesema Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Afya Bw. Englibert Kayombo

Amesema kuwa kupitishwa kwa muswada huu kutawezesha kila mtanzania kuwa ndani ya Mfumo wa Bima ya Afya hatua itakayoboresha zaidi upatikanaji wa huduma za matibabu bila kuwa na kiwazo cha fedha.

Serikali yetu ni sikivu sana na imefanyia kazi hoja zote zilizoibuliwa na Waheshimiwa Wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi hivyo yaliyomo ndani ya muswada huo yamelenga kuwasaidia wananchi kupata huduma bora za afya bila ya kikwazo cha fedha” alisema Bw. Kayombo.

Post a Comment

0 Comments