Ticker

7/recent/ticker-posts

MCHUNGAJI AJIUA KISA MAPENZI, AZIKWA BILA HESHIMA

Mchungaji  wa Kanisa la Pentekoste lililopo kwenye mji wa Nnewi nchini Nigeria, Prosper (30) aliyejiua kwa kujirusha kutoka ghorofa ya pili amezikwa juzi kwenye maeneo yasiyo na hadhi.

Hatua ya kuzikwa huko imetokana sheria ya mji wao, ambapo mtu anauejiua hastahili kuzikwa kwa heshima.

Imeelezwa kuwa sababu ya kujiua kwa mchubgaji huyo ni  wivu wa mapenzi. Ndugu wa mchungaji huyo alisema Prosper alitumia pesa nyingi sana kwa mwanamke aliyekuwa nae katika mahusiano ikiwemo kumsomesha chuo kikuu kwa makubaliano ya kuja kuoana wawe rasmi mke na mume

Ila baada ya hapo mdada husika akamsaliti mchungaji huyo pia kukataa kuolewa nae hali ambayo ilimpa mshtuko wa huzuni kubwa na kujiua ikifikiriwa pia gharama kubwa alizozitumia kwa muda mrefu.

Amejiua mwezi uliopita isipokuwa amezikwa Ijumaa hii kijijini kwao.

Post a Comment

0 Comments