Ticker

7/recent/ticker-posts

MUUMINI MWINJUNA AMLILIA ADOLF MBINGA

Mwanamuziki Muumini Mwinjuma

Mwanamuziki wa muziki wa dansi nchini Mwinjuna Muumini, ameguswa na kifo cha  mpiga solo mahiri nchini Adolph Mbinga alitlyefariki Dunia hivi karibuni.

Muumin aliyewahi kufanya kazi na Mbinga katika bendi ya Mchinga Sound ‘Kipepeo’,  amesema mwenzake huyo alikutwa na mauti  kijijini kwao Mpute , Wilaya ya Nachingwea.

“Nimepokea taarifa kutoka kwa kaka yake kwamba Mbinga alifariki jana usiku, ni msiba mkubwa kwa tasnia ya muziki wa dansi nchini,”amesema Muumin na kumuelezea marehemu Mbinga kama mtu aliyemsaidia kwa kiasi kikubwa katika masuala ya muziki nchini.

Mbinga atakumbukwa kwa umahiri wake katika gitaa la solo akiwa na bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ na albamu yao ya Kisa cha Mpemba, pia alikuwa kiongozi muasisi wa bendi ya Mchinga Sound na kushiriki katika albamu ya kwanza ya bendi hiyo iitwayo Kisiki cha Mpingo.


Marehemu Adolf Mbinga

Baadhi ya nyimbo alizotunga wakati wa uhai wake na kushiriki kupiga gita la solo ni Neema wa bendi ya Diamond Sound, Kisa cha Mpemba bendi ya Twanga Pepeta’, Mdomo, Binadamu na Mto Wenye Mamba bendi ya Mchinga Sound.

Post a Comment

0 Comments