Ticker

7/recent/ticker-posts

MZEE YUSUPH AMKATAA MTOTO WA NJE YA NDOA

Mwanamuziki wa muziki wa Taarab, Mzee Yusuph amemkataa waziwazi Ahmad Yusuph Mzee, anaedai kuwa yeye ni mtoto halali wa mwanamuziki huyo.

Ahmad amesema mama yake ambaye ni marehemu kwa sasa alipewa ujauzito na Mzee Yusuph wakati alipokuwa akihudumu kama MC kwenye moja ya kumbi iliyokuwa huko Mbagala, jijini Dar es Salaam mwaka 2002.

Ahmad anasema awali alikuwa akiishi na mama yake pamoja na mume wa mama yake ambaye alikuwa anamtambua kama baba yake mzazi, lakini kabla mama yake hajafariki alimweleza ukweli kwamba hakua baba yake wa kumzaa bali baba yake ni Mzee Yusuph ambaye ndiye ni mwimbaji wa taarabu.


Ahmad amesema licha ya kwamba anatambua kama Mzee ana mali za kutosha na ni mtu maarufu, yeye kipaumbele chake anataka wakapime DNA ajiridhishe kama kweli  ni baba yake mzazi ili awe na faraja pamoja na amani ya kujihisi yupo salama duniani kwani kwa maisha anayoishi sasa ni kwamba hana baba wala mama, maisha ambayo ni hatari na siyo kwamba anamtafuta ili apate upenyo wa kurithi mali.

Akizungumzia hilo, Mzee Yusuph pamoja na kuwa na mfanano na kijana huyo  amesema hamtambui kijana huyo kama mtoto wake na hana kumbukumbu kama aliwahi kucheza michezo ya hasara huko Mbagala kiasi cha kumpatia mwanamke ujauzito.


Awali Mzee Yusuph alikataa kabisa kupima DNA lakini baadae baada ya kushinikizwa alikubali kwenda kupima DNA lakini kwa masharti mazito, ambapo amesema kijana huyo akitaka wakapime DNA pesa ya vipimo aitafute mwenyewe kijana na andapo atakuta siyo mtoto wake basi hatua kali za kisheria za uzalilishaji zitachukuliwa dhidi yake, aidha Yusuph ameongeza kuwa kama akikuta mtoto huyo ni damu yake atamfikiria kama aendelee kumlea au aachane naye kwani dini yake inasema mtoto wa nje ya ndoa siyo mtoto wake ni wa mwanamke.

Post a Comment

0 Comments