Ticker

7/recent/ticker-posts

JEZI KUINUFAISHA ZAIDI SIMBA, YAINGIA MKATABA MNONO

Klabu ya Simba, imeachana na mzabuni wake wa jezi na vifaa vya michezo Fred Vunjabei na kuingia mkataba mpya na kampuni ya Sunderland The Only One.

Mkataba huo wa kusambaza vifaa vyote vya michezo vya klabu hiyo ni wa miaka miwili na thamani yake ni Sh. Bilioni 2 kwa mwaka na utakuwa ni wa kipindi cha miaka miwili.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula amesema angalau sasa Simba imeanza kufaidika na jezi zake.

"Mwanzoni tulikuwa tunapata milioni 400 kwa mwaka kutokana na jezi. Akaja Vunja Bei akatupa bilioni moja kwa mwaka na huyu wa sasa anakuja kutupa bilioni mbili kwa mwaka. Namshukuru sana Sandaland kwa kuwa mdhamini wa jezi kwa msimu wa 2023/24."



Post a Comment

0 Comments