Ticker

7/recent/ticker-posts

ESTER WA 'MWALIMU JIMMY' AMEPATIKANA

Hatimaye mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Pandahill Ester Noah Mwanyiru aliyetoweka shukeni hapo May 18,2023 amepatikana.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga  inaeleza kuwa  amepatikana kwenye eneo la Ifisi, lililopo Mji mdogo wa  Mbalizi kwa mama mfanyabiashara, Bi. Azrat Abdul Mohamed 

Mwanafunzi huyo alifika kwa mama huyo wiki mbili zilizopita akiwa na Joseph ambaye anafanya biashara ya mkaa.Jose alimuomba Azrat akae na binti huyo kwa madai kuwa ni mke wake na anamtafutia chumba cha kuishi. 

Alikaa kwa mama huyo hadi pale alipokutwa na makachero wa Polisi asubuhi ya leo.Wote wawili wapo kituo cha Polisi Mbalizi kutoa maelezo.

Jana Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera na Kamati ya Usalama ya Mkoa, wafanye uchunguzi zaidi na haraka kuhusu tukio la kupotea mwanafunzi Esther Mwanyiru aliyekuwa akisoma Shule ya Sekondari Panda Hill mkoani humo.


Majaliwa alitoa agizo hilo leo Juni 22, 2023 baada ya kupokea clip yenye maelezo ya mzazi wa binti huyo ambaye alikuwa akisoma kidato cha tano, tahsusi ya PCB shuleni hapo.

Katika clip hiyo, Mama mzazi wa Esther anadai yeye na mumewe waliitwa na uongozi wa shule hiyo, kujulishwa kwamba Esther hajaonekana tangu asubuhi Mei 18,2023.

Hadi sasa zimepita siku zaidi ya 20 wamekuwa wakimtafuta binti yao kila mahali bila mafanikio.

Mzazi huyo alidai Esther aliacha ujumbe wa maandishi akiwaaga rafiki zake na kuomba Mwalimu Jimmy aache kuwafanyia wanafunzi wengine kitendo alichomfanyia yeye kwani kimesababisha maisha yake kuwa magumu.

“Naomba umfikishie salamu Mwalimu Jimmy, mwambie ameyafanya maisha yangu kuwa magumu sana hapa shuleni.

“Asiendelee kuwafanyia wanafunzi wengine kama alivyoyafanya maisha yangu mimi kuwa magumu,” alisema mzazi huyo akisoma sehemu ya ujumbe huo.

Post a Comment

0 Comments