Ticker

7/recent/ticker-posts

WAZIRI MKUU ALITAKA BARAZA LA MICHEZO LA UMOJA WA AFRIKA KUKUZA MICHEZO

WAZIRI MKUU ALITAKA BARAZA LA MICHEZO LA UMOJA WA AFRIKA KUKUZA MICHEZO

Rais Dkt. Samia aipigia debe Tanzania ichaguliwe kuwa Makao Makuu ya Sekretariat ya Baraza hilo.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri wa michezo wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya Nne kuweka nguvu katika kuhakikisha wanakuza na kuendeleza michezo kwa Ukanda huo.

Amesema hayo leo Alhamisi (Mei 04, 2023) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa Michezo wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya IV Jijini Arusha.

Amewataka mawaziri hao wawekeze kwenye kujenga uwezo wa kitalaamu ili kuzalisha wanamichezo wanaoweza kuleta mageuzi kwenye Sekta ya Maendeleo ya Michezo na Maendeleo kupitia Michezo “Tusikubali kushika mkia kila siku na wala tusikubali kurudi nyuma”.

Amesema kuwa lengo la kila taifa ni kuona timu yake inashinda makombe ya Kimataifa hasa Kombe la Dunia. “Tukiamua kuwekeza kwenye miundombinu ya michezo na ujuzi pamoja na kushirikiana tunaweza kufikia malengo makubwa kwenye sekta ya michezo”

"Tunapaswa kufika mahali pa kuona kuwa Tanzania ikishinda wote tumeshinda, Uganda ikishinda, wote tumeshinda, Ethiopia ikishinda wote tumeshinda. Tushirikiane ili tuwe mfano na kielekezo kwa Kanda nyingine za Mabaraza ya Michezo ya Umoja wa Afrika”.

Katika Hatua nyingine, Waziri Mkuu  amewataka wajumbe wa mkutano huo kuichagua Tanzania kuwa makao makuu ya Sekretarieti ya Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Ukanda wa IV katika uchaguzi utakaofanyia mapema leo Mei 04, 2023.

Amewaeleza wajumbe hao kuwa Tanzania ina kila sababu ya kupigiwa kura ya ndiyo kutokana na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuipa hadhi sekta ya michezo nchini.

Amesema kuwa uwepo wa mageuzi makubwa katika diplomasia ya michezo ya kimataifa ambapo chini ya uongozi thabiti wa Serikali timu za Taifa za Tanzania na vilabu zinafanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa “jambo hili linatia hamasa kwa wanachama kuona kuwa Tanzania inapiga hatua katika kuendeleza sekta ya michezo nchini”

"Uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali kwenye miundombinu ya michezo ikiwemo ujenzi wa viwanja linaongeza ubora kwa nchi yetu."


Post a Comment

0 Comments