Ticker

7/recent/ticker-posts

MWANAMUZIKI WA NIGERIA AJITOA SADAKA

Mwimbaji na mtunzi mashuhuri wa Nigeria Chidnma ambaye alibadilika kutoka katika kuimba muziki wa kidunia hadi kuwa msanii wa Injili, amefichua kwamba alizaliwa na ulemavu wa macho.

Katika video iliyowekwa kwenye Chaneli yake ya YouTube anasema kwamba wazazi wake walikabiliana na changamoto kubwa katika kujaribu kushughulikia hali yake ya matibabu, na baada ya juhudi zao zote kushindwa walimgeukia Mungu.

Kwa muujiza alipata kuona tena, na mama yake bila yeye kujua akaweka nadhiri ya kumweka sadaka kwa Mungu kama tokeo.

Alibainisha kuwa licha ya kufumbua macho yake, mama yake alimjulisha kuwa yana rangi nyekundu ya damu, jambo ambalo likawa kero nyingine na kuwafanya wakose amani muda mwingi.

"Nilizaliwa kipofu kwa kweli, sikufumbua macho yangu hata kidogo na hiyo ikawa changamoto. Wazazi wangu walijaribu kila wawezalo kunifanya nione, bila mimi kujua mama yangu alifanya makubaliano na Mungu"- alisema

Ikumbukwe mnano Mei 2021, Chidinma alitangaza rasmi kwenye ukurasa wake wa Instagram mabadiriko yake kuelekea muziki wa injili na huduma ya Kikristo, japokuwa pia hata katika muziki wa kidunia alikuwa anafanya vizuri na alishilikiana na wasanii nguli wengi kutoka Nigeria.


Post a Comment

0 Comments