Ticker

7/recent/ticker-posts

KERR AITISHIA NYAU YANGA

Kocha wa Marumo Gallants ya Afrika Kusini aliyewahi kuifundisha Simba, Muingereza Dylan Kerr amefunguka kuwa ana uhakika mkubwa wa kupata matokeo katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe Shirikisho Afrika dhidi ya Yanga kwa kuwa atapata sapoti kubwa kutoka kwa Simba.

Marumo Gallants inatarajiwa kucheza na Yanga mchezo wa kwanza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika Mei 10, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar kabla ya mchezo wa marudiano unaotarajia kupigwa Mei 17, mwaka huu nchini Afrika Kusini.

 Kerr alisema kuwa anakuja Bongo kwa kazi ya kuhakikisha wanapata matokeo ya ushindi huku akaimini atapata sapoti kubwa kutoka kwa Simba ambao ni wapinzani wakubwa wa Yanga.

"Binafsi hatuna presha ya mchezo wetu na Yanga kwa sababu nawajua vizuri na tayari tumeanza kuwafuatilia kupitia watu wetu lakini siyo mgeni na Tanzania kwa kuwa tayari nimewahi kufanya kazi na Simba ambao ni familia yangu, malengo yetu kama timu ni kuona tunashinda kwa kupita kila hatua ya michuano hii mikubwa Afrika.


"Naamini matokeo ya ushindi ambayo tunatarajia kuyapata katika mchezo wa kwanza Tanzania, yatachagizwa na Simba pamoja mashabiki wao kwa sababu itakuwa ni furaha kubwa kuona tumewafunga wapinzani wao licha ya kwamba tunapita katika kipindi kigumu katika ligi ya nyumbani kwa kupambania kubakia katika ligi kuu lakini hatuwezi kusitisha malengo,” alisema Kerr.


Post a Comment

0 Comments