Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Tanzania inajivunia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kama mfano barani Afrika.
Ameyasema hayo leo Aprili 25, alipohutubia Kongamano la Miaka 59 ya kuadhimisha Muungano wa Tanzania lililofanyika ukumbi wa Idris Abdul-Wakil Kikwajuni, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amewashukuru watoa mada wa Kongamano hilo, Profesa Patrick Loch Otieno Lumumba kutoka Kenya kwa mada ya umuhimu wa Muungano na umoja katika bara la Afrika na Waziri mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Stephen Wassira kwa kuwasilisha mada ya historia ya umuhimu wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na Balozi Mohamed Hamza ambae mada yake ilijikita katika fursa zilizopo kwa vijana ndani ya Muungano.
Aidha Rais Dkt.Mwinyi amesema kuwepo kwa amani kwa taifa ni faida mojawapo ya Muungano kwa maendeleo alibainisha kuwa awamu zote zilizopita za utawala mpaka sasa zimekuwa zikidumisha uhusiano mwema, utamaduni, lugha fursa nyingi za ajira ushiriki wa siasa na kutumia rasimali zilizopo kwa pande zote mbili za Muungano.
0 Comments