Ticker

7/recent/ticker-posts

SIMULIZI LA MOTO NA PEPO

  Siku Moja Sayyedna Musa (A.S) alipokwenda kuzungumza na Mola Mlezi wa Ulimwengu wote 

Kwa Unyenyekevu mkubwa alimuuliza Ewe Mola wangu Mbona unawaumba Watu na kisha wengine unawachoma wengine unawaingiza peponi na wote umewaumba wewe"

Mwenyezi Mungu akataka kumfunza Nabii Musa kwa njia ya mfano  akamwambia Ewe Musa nenda Shambani kalime "

Sayyedna Musa akaenda shambani akalima mpaka ilipofika wakati wa mavuno akamwambiwa avune kisha alipovuna yale Mazao mazuri akachukua akayahifadhi kwenye ghala na yale mabua akayachoma Moto"

Mwenyezi Mungu akamwambia Ewe Musa ulichokifanya ndicho mimi nakifanya 

 Kama ulivyolima ,Ukapalilia,Ukavuna,na mazao mazuri ukayahifadhi kwenye ghala zuri na yale Mapepe akayachoma moto 

Nami ndivyo naumba kisha Wanaishi wale wenye Matendo Mazuri nawaingiza kwenye Pepo yangu na wale Wabaya wataingia Motoni "

In Shaaa ALLAH Watukufu ndugu zangu tumuombe ALLAH atupe Mwisho mwema nasi tuingie kwenye Janna yake baada ya Maisha yetu haya ya Dunia"

Post a Comment

0 Comments