Ticker

7/recent/ticker-posts

MANDONGA SASA KAMA 'BOB KILLER'

KARIM Mandonga,maarifu kama  mtu kazi, sasa amejijengea ufalme wa ndondi nchini Kenya huku akizitawala nchi waasisi wa  Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya na Uganda.

Kwa mara ya pili Mandonga ameweza kuitumia vema ardhi ya Kenya baada ya kufanikiwa kushinda mapambano yake yote mawili yaliyofanyika nchini humo.

Mchezo wake wa kwanza lilichezwa Januri mwaka huu dhidi ya Daniel Wanyonyi kwenye ukumbi wa KICC, ambapo aliibuka mshindi.


Bob Killer

Pambano lake la pili limechezwa juzi dhidi ya bondia wa Unganda, Kenneth Lukyamuzi kwenye uwanja wa kimataifa wa Kasarani, jijini Nairobi, ambapo pia ameibuka kidedea.

Ushindi huo unamfanya Mandonga kufananishwa na Simba mbabe wa Serengeti kwa sasa Bob Killer ambaye alifanikiwa kumuua aliyekuwa mbabe wa Serengeti Bob Junior.

Post a Comment

0 Comments