Ticker

7/recent/ticker-posts

USALAMA WAIMARISHWA KENYA

POLISI wameonekana kutanda maeneo kadhaa katika barabara kuu jijini Nairobi kabla ya maandamano yaliyopangwa na kiongozi wa Azimio, Raila Odinga.

Vyombo vya Habari nchini Kenya vimeripoti kuwa hekaheka zilianza usiku kwa Pilosi kuweka vizuizi barabarani na kukagua magari, kitendo ambacho kiliwatia hofu madereva wengi.

Mitaa mingi katikati ya jiji imesalia bila watu huku wafanyabiashara na wasafiri wakikaa mbali.

Kwa kawaida, mitaa ya jiji hujaa watu wanaoendelea na shughuli zao za kila siku. Wakazi wamedai kuwa askari waliokuwa doria waliwaambia watu kutokuwa katika mikusanyiko ya zaidi ya watu wawili.

Post a Comment

0 Comments