Ticker

7/recent/ticker-posts

RAIS DKT. SAMIA KUFANYA ZIARA YA KIHISTORIA URUSI

Kwa mara ya pili leo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anakwenda kufanya ziara ya kihistoria nchini Urusi tangu Tanganyika na baadae Tanzania kupata Uhuru mwaka 1961.

Ziara kama hii ya Rais Dkt. Samia iliwahi kufanywa na Rais wa Awamu ya Kwanza wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1969.

 

Katika kurasa zake za mitandao ya kijamii, Rais Dkt. Samia ameandika: Nimeondoka nchini leo kuelekea Shirikisho la Urusi kwa ziara ya Kitaifa kufuatia mwaliko wa Mheshimiwa Rais Vladimir Putin, ikiwa ni ziara ya pili kufanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya ile ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Oktoba 1969.

 

Ziara hii ni muhimu hasa tunapoelekea kuanza utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050 ambayo inataka ushiriki mkubwa wa sekta binafsi. Tutafanya mazungumzo na wenyeji wetu yanayolenga kuimarisha ushirikiano katika sekta za kimkakati zinazogusa maisha ya wananchi.

 

Aidha, tutashiriki majukwaa ya biashara na uwekezaji na kutatangaza fursa zilizopo nchini, pamoja na kufungua zaidi fursa za masoko kwa bidhaa za Tanzania nchini Urusi.



Post a Comment

0 Comments