Baadhi ya Waandishi wa Habari waliofanikiwa kushinda Tuzo maalum za TMDA za msimu wa mwaka 2024-2025.
NA JIMMY KIANGO
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imendelea na utaratibu wake wa kutoa tuzo maalum kwa Waandishi wa Habari ambao wameripoti taarifa na kuandaa Makala mbalimbali zinazohusu kazi na majukumu ya mamlaka hayo kwa kipindi cha mwaka mmoja ulioanzia Aprili 2025-Machi 2026.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa Machi 2026 na Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma, TMDA, lengo la Tuzo hizo ni kutambua mchango wa Waandishi wa habari na kuleta hamasa katika kuelimisha jamii kuhusu masuala ya udhibiti wa dawa, vifaa tiba, vitendanishi na bidhaa za tumbaku kupitia vyombo vya habari ili kulinda afya ya jamii.
“Napenda kuwatangazia Waandishi wa Habari kuwa TMD imeandaa Tuzo maalum kwa Waandishi ambao wameripoti taarifa na kuandaa Makala mbalimbali kuhusu kazi na majukumu ya TMDA katika kipindi cha kuanzia Aprili, 2025 mpaka Machi, 2026.
“Kazi zinazolengwa ni zile zilizoripotiwa kupitia runinga (TV), Redio, Magazeti na mitandao ya kijamii kwa kipindi tajwa, ambapo baada ya kupokelewa zitashindanishwa na hatimaye kupata washindi watakaopewa tuzo.
“TMDA inawaalika waandishi kuwasilisha kazi zao ifikapo au kabla ya tarehe 16 Aprili, 2026 kupitia anuani ya barua pepe ya commpedtmda@gmail.com au kwa njia ya CD katika ofisi za TMDA zilizopo Dodoma, Dar es salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Ruvuma, Tabora, Morogoro na Geita.”
0 Comments