Ticker

7/recent/ticker-posts

YANGA YAMALIZANA NA FIFA, SASA RUKSA KUSAJILI

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeiondolea Yanga adhabu ya kutosajli Wachezaji wapya baada ya kukamilisha malipo ya aliyekuwa Mchezaji wake Gael Bigirimana.

Awali mchezaji huyo alifungua kesi FIFA dhidi ya klabu hiyo ya Ligi Kuu ya NBC kwa kushindwa kumlipa baada ya kumvunjia mkataba.

Bigirimana alishinda kesi hiyo, na Yanga ilitakiwa kumlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo wa FIFA ulipotolewa lakini haikutekeleza na kusababisha ifungiwe kusajili.

Baada ya kukamilisha malipo hayo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nalo limeifungulia Yanga kufanya uhamisho wa ndani wa Wachezaji.

Post a Comment

0 Comments