Ticker

7/recent/ticker-posts

MAKONDA APEWA SALA NZITO NA MJANE WA HAYATI RAIS MAGUFULI

MAMA Janeth Magufuli ambaye ni mjane wa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Pombe Magufuli amempokea Paul Makonda nyumbani kwake Chato mkoani Geita na kumfanyia maombi maalumu ya kumtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi.

Pia Mama Janeth Magufuli alimsihi Makonda kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa bidii ili kufanikisha malengo ya  Rais Samia Suluhu Hassan ya kutimiza ilani ya chama.

Makonda anaendelea na ziara yake katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo jana Novemba 10, 2023 aliingia Chato mkoani Geita akitokea Bukoba na kutembelea kaburi la Hayati Magufuli pamoja na kuzungumza na wakazi wa Wilaya Chato.

Post a Comment

0 Comments