Ticker

7/recent/ticker-posts

TANZANIA KUREJESHA NCHINI RAIA WAKE WANAOISHI ISRAEL

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania imetoa taarifa ya kuwarejesha nyumbani Watanzania wote wanaoishi nchini Israel.

Hatua hiyo imekuja kutokana na  muendelezo wa mapigano kati ya Israel dhidi ya kikundi cha Hamas chenye makazi yake Palestina.

Taarifa hiyo imetolewa  leo Oktoba 14, 2023 kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa kufuatia kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama nchini Israel na maeneo mengine ya jirani, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeandaa mpango wa kuwarejesha nchini Watanzania waliopo nchini humo na maeneo mengine ya karibu. 

Serikali imefikia uamuzi huo baada ya kufanya tathmini na kujiridhisha kwamba mazingira ya sasa yanaruhusu zoezi hilo kufanyika. 

Hivyo, Watanzania walio tayari kurejea nyumbani wanashauriwa kujiandikisha kwenye Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Tel Aviv, Israel kupitia barua pepe: telaviv@nje.go.tz au simu namba: +972 533 044 978 na +972 507 650 072, kabla ya tarehe 15 Oktoba 2023, saa 6 usiku"

Post a Comment

0 Comments