Ticker

7/recent/ticker-posts

MWAKINYO KIZIMBANI, ADAIWA MAMILIONI YA SHILINGI

Kampuni ya PAF Promotion imefungua shauri dhidi ya bondia Hassan Mwakinyo ambalo linatarajiwa kutajwa kwa mara ya kwanza Novemba 13, 2023 katika Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam ambapo Kampuni hiyo imewasilisha kupitia wito wa kesi uliotolewa na Mahakama

Sehemu ya madai ya PAF dhidi ya Mwakinyo ni kumtaka aombe radhi kwa kugoma kupanda ulingoni na hivyo kukiuka mkataba wa kupigana Septemba 29, 2023. Pia, aombe radhi kwa kutoa taarifa za uongo kupitia vyombo vya Habari

Mengine ni pamoja na kulipa faini ya Tsh. Milioni 150 kama fidia ya madhara ya jumla yaliyosababishwa na kuahirishwa kwa pambano.

Post a Comment

0 Comments