Mjane wa aliyekuwa mfanyabiashara wa madini, Erasto Msuya, Miriam Mrita ameanza kujitetea katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
Miriam anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya wifi yake, Aneth Msuya alianza kujitetea jana mbele ya Jaji Edwin Kakolako na akadai kuwa aliteswa alipokuwa mikononi mwa polisi ili akiri kufanya mauaji hayo.
Mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni mfanyabiashara Revocatus Muyela.
Akiongozwa na Wakili Peter Kibatala, Miriam alidai Agosti 5, 2016 akiwa maeneo ya Tembo, Arusha akipata chakula mahali ambako hakupataja, walikwenda watu watatu na kumweka chini ya ulinzi.
0 Comments