Ticker

7/recent/ticker-posts

MKOA WA MANYARA UMEWEKA HOSTORIA

Mkoa wa Manyara umeweka historia ya kuwa mwenyeji wa matukio matatu ya Kitaifa ikiwemo uhitimishaji wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023, Ibada maalum ya Kumbukizi ya kifo cha Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa 2023.

Akizungumza na wanahabari katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Babati, Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga amesema kuwa mkoa umepata neema ya ajabu kwa kupata matukio makubwa ya kitaifa.

"Niwaombe Wananchi wa Mkoa wa Manyara pamoja na wageni wote kutoka nje ya mkoa wajitokeze kwa wingi, kwanza kumpokea Rais wetu mpendwa Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wote watakaoambatana nae katika mkoa wetu, vile vile niwaombe mjitokeze kwa wingi siku ya tukio lenyewe Katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Oktoba 14, 2023," amesema  Sendiga.

Mkoa wa Manyara umeanzishwa Agosti 2002 na Mkuu wake wa kwanza wa Mkoa alikuwa Kanali (mst) Anatolia Tarimo na sasa 2023 unaongozwa na Queen Cuthbert Sendiga.



Post a Comment

0 Comments