Ticker

7/recent/ticker-posts

IHEFU YAENDELEA KUVURUGA REKODI ZA YANGA

Ni Mbogo maji maarufu kama Ihefu, leo wameendelea kuzivuruga rekodi za Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Yanga kupitia kwa Pacome ndio ilianza kuwajeruhi Mbogo maji hao katika dakika ya nne ya mchezo. 

Ihefu walitulia na hatimae katika dakika ya 40 mlinzi wa timu hiyo Kissu alisawazisha na kuzipelekea mapumziko timu hizo zikiwa sare ya 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa Ihefu kulisakama lango la Yanga hadi dakika ya 67 pale Ilanfya alipounganisha krosi moja kwa moja langoni na kumwacha Diara akidaka hewa.

Matokeo hayo ya 2-1 yameifanya Ihefu kuvunja rekodi ya Yanga kucheza michezo mitatu ya Ligi Kuu bila kugungwa hata goli moja.

Ihefu ikiwa kwenye uwanja wake wa Highland Estate msimu uliopita iliivuruga rekodi ya Yanga ya kutofungwa katika micjezo yake zaidi ya 40 iliyocheza.

Post a Comment

0 Comments