Ticker

7/recent/ticker-posts

BARBARA ASHIRIKI KWENYE MAPOKEZI YA ARSENER WANGER

Mtendaji Mkuu wa zamani wa klabu ya Simba, Barbara Gonzalez ameshiriki kwenye mapokezi sanjari na kumkaribisha nchini, aliyekuwa kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ambaye kwa sasa ni Afisa Mkuu wa Maendeleo ya soka duniani.

Wenger amekabidhiwa wadhifa huo na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Wenger yupo nchini Tanzania na viongozi wengine wa FIFA kwa lengo la kushuhudia ufunguzi wa michuano mipya ya African Football League ambayo inazinduliwa leo na  klabu ya Simba ya Tanzania itacheza dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Post a Comment

0 Comments