Timu ya Simba sasa itaondolewa kwenye ratiba ya Ligi Kuu ya NBC kwa kipindi cha mwezi mmoja, kuanzia Oktoba 20 hadi Novemba 21,2023.
Uamuzi huo unatokana na matakwa ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) ambalo limelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuiondoa Simba kwenye ratiba ya ligi hiyo kwa kipindi hicho ili ipate nafasi ya kushiriki kikmilifu michuano ya CAF African Super League inayoshirikisha timu nane za ngazi ya klabu barani Afrika.
Ligi ya NBC inatarajiwa kianza kutimua vumbi Agosti 15 mwaka huu na kutamatika Mei 29,2024.
0 Comments