Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Yanga, wameongeza taji la ubingwa wa Kombe la Shiriksho la Azam, baada ya kuichapa bao 1-0 kwenye uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.
Yanga pamoja na kumkosa mpachika mabao wake mahiri, Fiston Mayele, iliweza kuimudu Azam Fc katika dakika zote za mchezo.
Bao la Yanga kwenye mchezo huo lilipachikwa na nyota wao raia wa Zambia Kenned Musonda katika dakika ya 13.
Bao hilo lililofungwa kwa kichwa lilidimu katika dakika zote za mchezo.
Yanga imefanikiwa kuchukua taji hili mara mbili mfululizo na kuendelea kujiwekea rekodi muhimu katika soka kwa msimu huu.
Yanga imekuwa na msimu mzuri baada ya kuanza kwa kunyakua uahindi wa ngao ya hisani, kombe la Ligi Kuu, mshindi wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika na sasa ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam.
0 Comments