Ticker

7/recent/ticker-posts

MUZIKI WA DANSI WAPATA PIGO

Mwanamuziki Kaposhoo enzi za uhai wake.


Mwanamuziki na mpiga tumba wa bendi ya Tukuyu Sound, Kaposhoo amefariki kwa ajali ya bajaji ambayo iligongwa na gari ndogo Kawe, mbele kidogo ya mzunguko wa Maringo jijini Dar es Salaam, alfajiri ya Jumapili ya Aprili 30,2023.

Kaposhoo alikuwa mmoja wa abiria waliokuwemo kwenye bajaji ambapo walifariki watu watatu akiwemo yeye.

Mwili wa Kaposhoo uko chumba cha kuhifadhi maiti Hospitali ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

Ndugu wa marehemu akiwemo mama yake mzazi wameridhia Kaposhoo kuzikwa Dar es Salaam kwa siku itakayotajwa baadae.

Mama wa marehemu atakuja Dsr es Salaam kushiriki mazishi ya mwanae.

Msiba wa Kaposhoo upo makao makuu ya bendi ya Tukuyu Sound, Mawasiliano Park, Ubungo.

Taarifa zaidi zitatolewa baadae ila kwa sasa taratibu za kipolisi zinaendelea kufanyika.

Rhobi Chacha, Kalala Jr, Said Mdoe, Papii Kocha na ndugu wa wawili wa marehemu wamekuwa wakishirikiana na polisi tangu asubuhi.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa Said Mdoe


Post a Comment

0 Comments