Ticker

7/recent/ticker-posts

TUNASAHAU WA KUJIPIMA NAO AU HATUJUI TUNASHINDANA NA NANI

@AlbogastBM

Miezi kadhaa nyuma ndugu yangu @alikamwe kwenye Camera na Vinasa sauti vya Azam TV angeweza kushauri kama alivyoshauri hapo ndugu yangu @yahyanjenge anayefanya hivyo kila siku kwenye vinasa sauti vya Clouds.

Nadhani sio mbaya kabisa tukiendelea kujua kuwa hakuna kipindi bora zaidi kwenye soka la Simba na Yanga kama hiki. Simba walianzisha hii safari 2018-19 sasa Yanga wamepunguza gepu la ubora wanachodaiwa ni consistency.

Na hapa nazungumzia ile tofauti ya kushiriki msimu mmoja ukashoot mpaka final na ukapotea kwa misimu 10. Timu zetu bado zina bajeti ndogo sana ukilinganisha na daraja la timu zinazoanza msimu zikitabiriwa ubingwa kama Mamelodi, Al Ahly, Esperance, Wydad na Raja.

Maana yake Simba na Yanga kimataifa hawashindani. Washindani wao ni mabingwa kama hao niliowataja hapo juu.

Robo fainali 4 za Simba SC anakutana na kipimo cha bingwa na anashindwa kuwatoa.

Alitolewa na TP Mazembe ambaye ni bingwa mara tano na alikuwa bado kwenye ubora wa kuwania ubingwa. Misimu kadhaa mbele Simba ameongeza ubora hawezi tena kutolewa na TP Mazembe.

Akatolewa na Kaizer Chief ambaye alienda fainali maana yake msimu huo Kaizer alikuwa na Class ya kuwa bingwa na alifungwa fainali na Al Ahly iliyokuwa bora zaidi. Misimu miwili mbele Simba sio tena ya kutolewa na Kaizer Chief.

Akatolewa na Orlando Pirates ambaye alienda fainali akafungwa na RS Berkane. Maana yake bado Simba anakwamishwa na timu za level ya ubingwa. Msimu mmoja mbele Simba hawezi tena kutolewa na Orlando Pirates.

Daraja la Simba kwenye robo fainali liko palepale ila Class ya ubingwa wa Afrika bado. Ubingwa wa Afrika unaenda kwa timu bora 5 za juu na Simba bado hajapenya kwenye hilo kundi la timu tano bora.

Nimechaguaga kumsikiliza zaidi @moodewji ambapo kabla na baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Wydad alisema Tuna kazi ya kuitoa timu kwenye Top 10 iingie kwenye Top 5 na hapo tutafanikiwa kuleta ubingwa wa Afrika.

Ukifanya tathmini ya wapinzani wa Simba SC robo fainali wote hakuna aliyeishia nusu fainali maana yake mtego wa Simba sio nusu fainali ni fainali na ubingwa. Usajili wa Simba unatakiwa kuwa wa Top 5 club sio Top 10.

Post a Comment

0 Comments