Ticker

7/recent/ticker-posts

TANZANIA YAPOKEA VIONGOZI WA JUU WA MATAIFA MATATU

Tanzania imeendelea kutembelewa na ugeni mkubwa wa viongozi kutoka nchi tatu kwa mwezi huu wa Januari pamoja na Februari lengo likiwa ni kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kati ya Tanzania na mataifa mengine. Leo Januari 22, 2024,nchi imempokea Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China Liu Guozhong aliyekuja nchini kwa ziara ya siku tatu. Katikati ya ujio wa kiongozi huyo wa China, kesho Januari 23, 2024 Tanzania itapata ugeni mwingine wa Makamu wa Rais wa Cuba, Salvador Valdes Mesa atakayekaa nchini kwa siku tatu lengo likiwa ni kukuza mahusiano ya nchi hizi mbili. Baadhi ya mambo atakayofanya Valdes ni kutembelea kiwanda kinachozalisha dawa ya Biolarvicide cha Kibaha na kusalimiana na Watanzania waliosoma Cuba. Rais wa Jamhuri ya Poland, Andrzej Duda anatarajia kuwa na ziara ya kikazi Februati 8 na 9, 2024 katika hatua ya kuimarisha diplomasia ya Tanzanua na Poland ambao wana uhusiano mzuri katika miradi ya maendeleo ya miundombinu, uhifadhi wa wanyama pori, elimu, maji na usimamizi wa mazingira, utalii, biashara na uwekezaji bila kusahau ushirikiano wa mabunge. Aidha Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amealikwa kufanya ziara za Kitaifa Indonesia, Vatican na Norway.

Post a Comment

0 Comments